Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UN News

Makala Maalum

Utamaduni na Elimu Nchini Burkina Faso, ufadhili kutoka Mfuko wa Elimu Haiwezi Kusubiri au Education Cannot Wait, wadau wa elimu duniani likiwemo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF na wadau wa kimkakati wanawarejesha shuleni wasichana na wavulana. Wanarejeshwa maeneo salama wanakoweza kujifunza kwa njia mbali mbali ikiwemo kupitia vipindi vya redio. Wakipatiwa  mafunzo kama ya ufundi ili hatimaye wajifunze kile walichokosa.

Habari Nyinginezo

Amani na Usalama Mapigano makali yanayoendelea kaskazini mwa Gaza yamelazimu watu wapatao 84,000 kukimbia eneo la mashariki la mji wa Gaza ndani ya siku chache, huku mapigano hayo yakisababisha pia kukatika kwa mawasiliano na eneo muhimu linalohusika na usambazaji wa misaada, yamesema mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayotoa misaada ya kibinadamu eneo hilo.
Amani na Usalama Afisa Mwandamizi wa jeshi la Sudan Kusini, Brigedia Jenerali Liep Bol Lam amewaomba wananchi wa Sudan Kusini kuungana pamoja ili kujenga taifa hilo.